Habari

Sherehe ya Wanawake Duniani

Sherehe ya Wanawake Duniani

Sherehe za siku ya Wanawake DUNIANI ambazo hufanyika Kila mwaka tarehe 8 March Duniani kwa Chama Cha Wafanyakazi RAAWU huwa zinaambatana na ufanyaji wa matendo ya Huruma,

Kama vile kutoa misaada kwa jamii kwa kutembelea wagonjwa mahospitarini, kutembelea wafungwa, kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ya wazi, utoa Elimu mbalimbali kwa wanachama Wanawake kuhusu masuala ya Jinsia, Afya, ujasiliamali, Sheria za kazi nk

Mwaka huu 2022, pamoja na shughuli nyingi zilizofanywa na wanachama Wanawake wa Kila mkoa , RAAWU TAIFA ilitembelea wagonjwa katika hospitali ya Ocean Road Dar es salaam na kutoa msaada kidogo wa sabuni na maji kwa wagonjwa.

Hata hivyo Kamati hii ya Wanawake Taifa inaomba inapenda kuona matendo ya Huruma kwa jamii yanafanywa Mara kwa Mara na wanachama wake pasipo kusubiri mpaka wakati wa MAADHIMISHO hayo.

 Wakwanza kutoka kushoto ni Mwenyekiti Wanawake RAAWU TAIFA Bi. Magdalena Mpanda akifuatana na Mratibu wa Jinsia wa RAAWU Bi. Mariam Mgalula

KARIBU RAAWU

Makao Makuu

  • Bibi Titi/Sophia Kawawa Street
  • P. O. Box 22532 Dar-es-Salaam
  • Tel: +255-22-2123762
  • Fax: +255-22-2123762
  • Email: info@raawu.or.tz
  • Website: www.raawu.or.tz